Siku moja baada ya msanii wa Bongo Fleva Mario kutoa wimbo wake Oluwa ambao uko kwenye Album ya The God Son,Msanii Marioo ameonyesha shukrani za dhati kwa mashabiki wake kufuatia mapokezi makubwa ya wimbo huo.
Mario amechapisha kwenye Instagram, ameeleza kuwa upendo anaoupata si wa kawaida, akisema wazi kuwa mashabiki wake wameamua asife njaa, kauli iliyojaa unyenyekevu na kuthamini mchango wa wanaomuunga mkono.
Ndani ya muda mfupi tangu kutolewa, OLUWA imekusanya maelfu ya watazamaji na maoni chanya, jambo linaloonesha nguvu ya mahusiano kati ya msanii na mashabiki. Marioo amesisitiza kuwa mafanikio hayo si kwa ujanja wala mbinu, bali ni matokeo ya imani na mapenzi ya kweli kutoka kwa watu wake.
Kauli hiyo inawapa mashabiki hisia ya kuthaminiwa, huku ikionyesha upande wa msanii anayeelewa kuwa muziki unaishi kwa sababu ya wanaousikiliza. Kwa OLUWA, marioo_tz hajaachia wimbo mpya, bali ameimarisha uhusiano, akithibitisha kuwa shukrani na unyenyekevu vina nafasi kubwa pale Sanaa inapokuwa njia panda.