Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo, anatarajiwa kuanza ziara rasmi katika mataifa manne ya Afrika kuanzia Aprili 13 hadi 23, 2026, ikiwa ni safari yake ya tatu ya kitume nje ya Italia tangu aanze uongozi wake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Holy See Press Office, Papa Leo atatembelea mataifa ya Algeria, Cameroon, Angola na Equatorial Guinea katika safari ya siku 11 itakayohusisha hotuba 10, mahubiri nane na salamu sita katika miji 11.
Ziara hiyo inafuatia safari yake ya mwaka 2025 katika Mashariki ya Kati alipokwenda Uturuki na Lebanon, huku safari nyingine ya Ulaya ikitarajiwa kufanyika Machi 28 mwaka huu katika Monaco.
Ratiba inaonyesha Papa Leo ataanza ziara yake katika Algeria, ambapo anatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Algiers Aprili 13.
