Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita, amewataka madiwani wa Manispaaya Shinyanga kutanguliza maslahi ya wananchi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mhita ametoa agizo hilo katika kikao kazi cha madiwani na wakuu waidara katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwakumbusha mambo muhimu wanayo paswa kuzingatia wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Amesisitiza kuwa madiwani ni daraja kati ya wananchi na Serikali hivyo wanapaswa kusikiliza na kutatua kero zao kupitia mikutano ya hadhara na kuzipeleka serikalini kwa ufumbuzi.
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Pendo Sawa, ameahidi kutekeleza maagizo waliyo pewa na kufanya kazi kwa ushirikiano kuongeza ukusanyaji wamapato na kuchochea maendeleo.
Mafunzo kwa madiwani hufanyika kila wanapoingia madarakani kuwawezesha kutekeleza majukumu ya uwakilishi nausimamizi wa shughuli za maendeleo.