Mtayarishaji wa muziki nchini Tanzania, Mr. T Touch, ameelezea hali ilivyo kwa malipo ya watayarishaji wa muziki (producers) ndani ya kiwanda cha nchini, akigusia changamoto anazoona zinaendelea licha ya muziki kuingiza fedha na kubadilisha maisha ya wasanii wengi.
Kupitia Instastory yake, Mr. T Touch amedai kuwa mpaka sasa Tanzania hakuna msanii anayekubali kulipa Shilingi Milioni 10 kwa studio session, wakati baadhi ya nyimbo zilizorekodiwa zimewaingizia wasanii mapato makubwa.
Aidha, ameeleza kuwa producers wanapodai haki zao mara nyingi hukutana na mazingira magumu kutoka kwa wasanii.
Touch ameandika “Eti bongo mpaka sahivi hakuna msanii anayeweza kulipa M10 kwa studio session wakati hizo audio wengi tu zimewaingizia hela nyingi na zimewabadilisha maisha, bado producers wakidai haki zao msanii anaingilia huku anatokea huku, bado tupo kwenye kuchonga barabara. Kwakweli madogo tuendelee kukaza lakini ukweli ndo huo.”
