
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa taarifa yake mpya kuwa Viwango vya vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga barani Afrika vimepungua tangu mwaka 2000.
WHO imesema aifa Kati ya mwaka 2000 na 2020, vifo vya akina mama katika ukanda wa Afrika vilipungua kwa asilimia 40, kutoka vifo 727 hadi 442 kwa kila vizazi hai 100,000,.
Hata hivyo, kasi ya kupungua kwa vifo hivyo bado haitoshi kufikia lengo la Maendeleo Endelevu (SDG) la kuwa na vifo chini ya 70 kwa kila vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2030.
Kaimu Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika Dkt. Chikwe Ihekweazu amesema zaidi ya asilimia 60 ya nchi za Afrika sasa zinaripoti kuwa zaidi ya asilimia 80 ya watoto huzaliwa kwa msaada wa wahudumu wa afya wenye ujuzi, ongezeko kutoka asilimia 28 mwaka 2010.
Aidha Dkt. Ihekweazu amesema pamoja mafanikio hayo, bado kuna mapengo makubwa hasa katika maeneo ya vijijini na yale yaliyoathiriwa na migogoro.