Uwanja kwa mwezi Februari kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.
Katika hatua nyingine Ramadhan Karanje wa B19 amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Februari wa Ligi ya NBC Championship 2025/26, huku Mbwana Makata wa Polisi Tanzania akichaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Karanje aliyeingia fainali na Obrey Chirwa wa Kagera Sugar na Tariq Seif wa Polisi Tanzania, alionesha kiwango chenye mwendelezo ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne (4) kwa dakika 404 za michezo mitano aliyocheza.
Kwa upande wa Makata aliyeingia fainali na Juma Kaseja wa Kagera Sugar na Zuberi Katwila wa Geita Gold, aliiwezesha timu yake kushinda michezo minne na kutoka sare mmoja hivyo kupanda kutoka nafasi ya sita hadi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ya NBC Championship.
