Serikali ya Tanzania imeondoa Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) kwenye uagizaji wa mitungi ya gesi (LPG), mitungi mikubwa ya gesi (LPG Bulk Facility na carbonizers za kutengeneza mkaa mbadala.
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na Serikali kupunguza bei na kurahisisha upatikanaji wa nishati safi ya kupikia kwa wananchi wakati akifungua Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililoandaliwa na wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau mkoani Morogoro.
“Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassan ameweka kipaumbele katika kuhakikisha nishati safi ya kupikia inapatikana kwa wananchi kupitia upatikanaji wa mitungi ya gesi, majiko banifu, gesi vunde na kupitia usambazaji wa umeme hadi ngazi ya vitongoji.” Amesema.
Ndejembi amesema mpango huo wa Rais Samia unawezesha matumizi ya nishati ya umeme katika kupikia ambapo mpaka sasa Tanesco kupitia kampuni ya MECS imewezesha wateja 480 kupata majiko ya kupikia kwa umeme kwa kulipia kidogokidogo kupitia bili za umeme.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema ajenda ya nishati safi ya kupikia ni kwa ajili ya maendeleo endelevu ya wananchi na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuifanya kuwa ni ya kitaifa na kuwataka wananchi kuiunga.
