Naomi Milton- KIGOMA
Shirika la Umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Kigoma limepokea vitendea kazi kutoka serikallini ikiwemo magari 5 bajaji 5 na pikipiki 11 ambavyo vitasaidia kuboresha utendaji kazi wa shirika hilo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa vitendea kazi hivyo Mkuu wa wilaya ya Kigoma Rashid Chuachua kwa Niaba ya Mkuu wa mkoa Balozi Simon Sirro amewataka Tanesco kuvitunza vifaa hivyo ili vidumu na Kusaidia kuimarisha shughuli za shirika hilo.
DC Chuachua ameongeza kuwa zaidi ya vitongoji 316 mkoani Kigoma vinatarajia kupata umeme ambapo serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 54 ili kusaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.

Akitoa taarifa baada ya kupokea vitendea kazi hivyo kaimu meneja Tanesco Mkoa wa Kigoma Mhandisi Hassan Nganjau ameishukuru serikali kwa kuliona hilo kwani awali walifanya kazi katika mazingira magumu lakini sasa wana uhakika wa kuwafikia wateja kwa wakati katika mazingira yoyote ya mjini na vijijini.
Wilaya zilizopokea vifaa hivyo ni pamoja na Kasulu, Uvinza, Kakonko, Kibondo na Kigoma mjini.
