Mahakama nchini Marekani imeamuru kituo cha habari cha Voice of America V.O.A kirejee kurusha matangazo na kwamba amri ya utawala wa Donald Trump ya kukifunga ilikuwa kinyume cha sheria
Jaji wa Mahakama ya Wilaya Royce Lambert amekipa chombo hicho cha kimataifa wiki moja kuendelea kutangaza huku akiamuru kurudi kazini kwa mamia ya waandishi wake.
V.O.A iliundwa wakati wa Vita vya dunia vya pili ili kukabiliana na propaganda za Wajerumani wa Nazi.
Donald Trump aliamuru kufungwa kwa chombo hicho cha habari wiki chache tu baada ya kurejea ofisini Januari 2025 ambapo maafisa katika utawala wake wameishutumu V.O.A kwa kuwa na mielekeo ya mrengo wa kushoto.
Wakati huo huo, Donald Trump pia aliamuru shughuli za vyombo vya habari kama vile Radio Free Europe na Radio Free Asia kuzimwa.
