Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe, ametoa tamko rasmi kufuatia uamuzi mzito wa Bodi ya Rufaa ya CAF kuivua Senegal ubingwa wa AFCON 2025 na kuukabidhi kwa Morocco.
Bodi ya Rufaa imebatilisha ushindi wa Senegal wa 1-0 uliopatikana uwanjani mwezi Januari na kuipa Morocco ushindi wa 3-0 wa mezani (forfeit).
Hii ni kutokana na kitendo cha wachezaji wa Senegal kugoma na kutoka nje ya uwanja kwa dakika kadhaa kupinga penalti wakati wa mchezo wa fainali.

Motsepe amesisitiza kuwa uamuzi wa Bodi huru ya Rufaa lazima uheshimiwe, akisifu viwango vya juu na weledi wa bodi hiyo.
Haki ya Senegal: Amebariki mpango wa Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) kwenda kukata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) huko Uswisi.
Motsepe ameahidi kuwa CAF itaheshimu uamuzi wowote utakaotolewa na CAS kama chombo cha juu kabisa cha kisheria michezoni.
