Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) imesema maonesho ya elimu ya mazingira yatafanyika Machi 28–29 katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, yakilenga kuonesha namna taka zinavyoweza kugeuzwa kuwa rasilimali kupitia ubunifu na urejelezaji.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa maonesho hayo yatatangulia kilele cha Siku ya Kuondoa Taka Duniani kinachotarajiwa kufanyika Machi 30, ambapo taasisi za serikali, sekta binafsi na wadau wa mazingira watashiriki kutoa elimu kuhusu usimamizi bora wa taka.
