Mkuu wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera Dkt. Abel Nyamahanga ameziagiza taasisi zote zinazolisha watu zaidi ya 100 kuanza matumizi ya nishati safi ndani ya kipindi cha miezi miwili.
Ametoa agizo hilo March 24,2026 ikiwa ni sehemu ya juhudi za kulinda mazingira na kuhifadhi misitu ambayo imekuwa ikiharibiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na matumizi ya kuni na mkaa.
Dkt. Nyamahanga amesema hatua hiyo inalenga kupunguza ukataji holela wa miti pamoja na kuchangia katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi hivyo amezitaka taasisi husika kuhakikisha zinazingatia maelekezo hayo kwa wakati.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Muleba wameshauri elimu zaidi iendelee kutolewa kwenye jamii juu ya umuhimu wa kutumia nishati safi ili kulinda mazingira.
