Safari ya Arne Slot ndani ya Liverpool inaonekana kufika ukingoni! Wakala wa Xabi Alonso, Inaki Ibanez, amethibitisha kuwa klabu ya Liverpool tayari imewasiliana naye kuulizia uwezekano wa fundi huyo kurithi mikoba ya Slot klabuni hapo.
Baada ya kuiongoza Liverpool kutwaa ubingwa msimu uliopita, mambo yamegeuka kwa Slot msimu huu ambapo Majogoo wamepoteza mechi 10 za EPL rekodi mbaya zaidi tangu msimu wa 2015-16.

Mambo muhimu kuhusu dili hili:
โข Mawasiliano Yameanza: Mtendaji mkuu wa Liverpool, Michael Edwards, ameweka nguvu zote kuhakikisha Alonso anarejea Anfield msimu ujao.
โข Sharti la Xabi: Alonso ameweka msimamo kuwa anataka kuwa na sauti ya mwisho kwenye usajili na masuala ya ufundi, jambo ambalo lilikuwa gumu alipokuwa Real Madrid.
โข Muda wa Kuwasili: Alonso hana mpango wa kuchukua timu katikati ya msimu; badala yake, anatarajiwa kuanza kazi katika dirisha la majira ya kiangazi.
Alonso amekuwa kipaumbele namba moja kufuatia mafanikio yake makubwa aliyoyapata akiwa na Bayer Leverkusen kabla ya kwenda Real Madrid.
