Chuo Kikuu cha Ulster (UU) kiliweka zulia jekundu maalumu kwajili ya Schwarzenegger siku ya Jumatatu ya jana na kumpa shahada ya heshima mwanasiasa huyo na nyota wa tasnia ya uigizaji Marekani.
Schwarzenegger alisema anakumbuka tukio la ziara yake ya kwanza kabisa mjini Belfast ilikuwa ni mwaka 1966, ilikuwa ni mafanikio kwake kwa sababu ilikuwa mara ya kwanza alialikwa kuzungumza hadharani, ilimjengea kujiamini.
Tukio zima la kupewa heshima ya udaktari katika mji huu ambao ameukanyaga kwa mara ya pili toka mwaka 1966 lilimtoa chozi la furaha.
Belfast ni mji mkuu na mji mkubwa zaidi wa Ireland ya Kaskazini, unaojulikana kwa urithi wake wa viwanda, haswa kama mahali pa kuzaliwa kwa RMS Titanic, na utamaduni wake mzuri na wa kipekee.
Wanafunzi wa chuo cha Ulster walishangilia na kushika mabango yaliyosomeka “Ulster, he is back” “Hasta La Vista, Ulster”, huku baadhi wakileta nakala za filamu yake Terminator 2 kuonyesha mapenzi makubwa kwa mwigizaji huyu nguli kabisa katika tasnia ya uigizaji Marekani.
Gavana huyu wa zamani wa jimbo la California alisema: “Chuo Kikuu cha Ulster ni chuo kikuu muhimu sana, na daima ni heshima kubwa kuheshimiwa hivyo.
