Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya petroli nchini kuanzia leo asubuhi, bei zikiongezeka kutokana na hali ya soko la kimataifa.
Bei hizo zinaanza kutumika leo Jumatano Aprili mosi, 2026. Hatua ya kupanda ni kutokana na mapigano yanayoendelea Mashariki ya Kati kati ya Marekani na Israel na Iran.
Kwa mujibu wa Jedwali la Bei Kikomo za Rejareja, bei mpya za mafuta katika Mikoa ya Kigoma, Kagera, Mwanza, Shinyanga, na Geita zimeongezeka.
Mkoa wa Kagera, bei ya petroli inauzwa kati ya shilingi 4045 hadi 4080, dizeli shilingi 4,030 hadi 4066, na mafuta ya taa yanauzwa kwa shilingi shilingi 3,909 hadi 3,945 kwa lita.
Mkoa wa Kigoma petroli inauzwa kati ya shilingi 4,017 na 4024, dizeli shilingi 4003 hadi 3032, na mafuta ya taa shilingi 3,882 na 3,891 kwa lita moja.
Mkoa wa Geita petroli inauzwa kati ya shilingi 4,054 hadi 4020, dizeli shilingi 4044 hadi 30935, na mafuta ya taa shilingi 3,906 na 3,874 kwa lita moja.
Mkoa wa mwanza petroli inauzwa kati ya shilingi 4,064 hadi 3999, dizeli shilingi 4050 hadi 3985, na mafuta ya taa shilingi 3,929 na 3,855 kwa lita moja.
Mkoa wa Shinyanga petroli inauzwa kati ya shilingi 4,003 hadi 3981, dizeli shilingi 3989 hadi 3967, na mafuta ya taa shilingi 3,867 na 3,864 kwa lita moja.
Ewura imetangaza bei mpya ya mafuta ambapo kwa Jiji la Dar la Salaam, Petroli imepanda kwa Sh956 kwa lita kutoka Sh2864 Machi hadi Sh3820 Aprili.
Kutokana na hali hiyo, sasa wanunuaji wa mafuta kwa bei ra rejareja yanayopitia Bandari ya Dar es Salaam watalazimika kuongeza Sh956 katika kila lita moja ya mafuta baada ya bei kufikia Sh3,820 kutoka Sh2864.
EWURA imesema kuwa ongezeko la bei ni janga la kidunia ambalo Tanzania haina uwezo wa kulidhibiti, na imechukua hatua za kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nakuwataka wananchi kutumia mafuta kwa uangalifu.
Ongezeko hili limetokana na vita vinavyoendelea kati ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ambavyo vimeathiri uzalishaji wa mafuta na kusababisha kufungwa kwa mlango wa Hormuz, kuongezeka kwa gharama za usafirishaji na bima za meli.
