Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra), Habibu Suluo amewataka waendeshaji wa vyombo vya moto kufuata taratibu zilizowekwa kabla ya kufanya mabadiliko yoyote ya nauli.
Amesena ongezeko lisiloidhinishwa linaweka mzigo usio wa haki kwa abiria.
Ametoa kauli hiyo ikiwa ni saa chache tangu kutangazwa kwa bei mpya za mafuta zilizoanza kutumika leo Jumatano, Aprili mosi 2026 ambazo zimeibua malalamiko katika maeneo tofauti ikiwemo mitandao ya kijamii.
Pia kutangazwa kwa bei hizo kumechochea kupandishwa kwa nauli katika baadhi ya maeneo jambo lililoongeza mzigo kwa wananchi.
Suluo amesema wanatambua bei za petroli na dizeli zimepanda Dar es Salaam na baadhi ya waendeshaji tayari wamepandisha nauli bila kibali licha ya kuwa mabadiliko yoyote lazima yazingatie kanuni,” amesema.
Kufuatia hali hiyo, amesema Latra itafanya kikao cha wadau Aprili 8, 2026 jijini Dar es Salaam, ambacho pia kitarushwa mtandaoni ili kuwashirikisha watu wengi zaidi.
