Na William Mpanju- Biharamulo, KAGERA
Serikali imeshauriwa kuchukua hatua za makusudi katika kufufua vivutio vya utalii vilivyopo kwenye halmashauri mbalimbali ili kuongeza mchango wake katika uchumi wa taifa.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Chuo cha Utalii Kagera kilichopo Biharamulo, Bw. Stanley Thomas, wakati wa ziara ya wanafunzi waliotembelea maporomoko ya mto Kisuma yaliyopo kijiji cha Katerela, kata ya Ruziba.
Amesema uwekezaji katika vivutio hivyo unaweza kusaidia kuongeza mapato ya ndani pamoja na fedha za kigeni, lakini bado kuna changamoto za miundombinu na uendelezaji.
