Msanii wa hip hop, Truba TZ, amesema wasanii wa Bongo Fleva mara nyingi huwa na tabia ya kulalamika zaidi kuliko wasanii wa hip hop.
Akizungumzia tasnia ya muziki, Truba amesema kila msanii aliyefanikiwa amewahi kupata msaada kutoka kwa mtu katika safari yake ya mafanikio. Pia amehoji sababu ya baadhi ya wasanii, akimtaja Harmonize, kuendelea kumlaumu Diamond Platnumz licha ya historia yao ya kufanya kazi pamoja.
Kwa upande mwingine, Truba amesema muziki wa hip hop una nafasi kubwa ya kupenya katika soko la kimataifa. Ameongeza kuwa amefanya kazi mpya kwa kushirikiana na G Nako, akieleza kuwa mradi huo unaakisi dira yake ya kuipeleka hip hop kwenye viwango vya kimataifa.
