Mbunge wa Kigoma Mjini, Baba Levo, amewasihi vijana wa Kigoma kutokubali kushawishiwa na mtu yeyote kufanya vurugu.
Akizungumza kwenye jukwaa la Nandy Festival 2026, Baba Levo amesema amani ni msingi muhimu wa maendeleo na ustawi wa wananchi, hivyo ni jukumu la kila kijana kuilinda.
Amesisitiza kuwa vijana wanapaswa kutumia nguvu na uwezo wao katika shughuli za maendeleo badala ya kujihusisha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama na utulivu wa jamii.
Aidha, ametoa wito kwa wakazi wa Kigoma kuendelea kudumisha mshikamano na amani, akieleza kuwa utulivu wa eneo hilo ni muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
