Serikali ya Iran imetangaza kuanza kwa maombolezo ya siku tatu kufuatia kifo cha kiongozi mkuu wa nchi hiyo, Ayatollah Khamenei, huku hafla kuu ikitarajiwa kufanyika katika uwanja wa sala wa Imam Khomeini Mosalla mjini Tehran.
Hayo yamebainishwa Machi 4, 2026 katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, ambapo yanatarajiwa kuanza leo usiku.
Waombolezaji na wafuasi wa kiongozi huyo wanatarajiwa kukusanyika katika uwanja huo maarufu uliopo mji mkuu wa Iran, kwa ajili ya kumuaga rasmi kiongozi huyo aliyekuwa na ushawishi mkubwa katika siasa na masuala ya kidini ya taifa hilo.
Tangazo hilo limekuja wakati hali ya usalama ikiendelea kuwa tete kufuatia mashambulizi ya anga yanayoendelea kufanywa na Israel kwa kushirikiana na Marekani.
