Na Shafiru Yusufu- Muleba, Kagera
Wanawake wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera wametoa msaada mahitaji mbalimbali kwa makundi maaalum ikiwemo viti mwendo 10 kwa watu wenye ulemavu na mahitaji ya familia kwenye kaya 20 za watoto wanaojilea wao wenyewe.
Misaada hiyo imekabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Muleba Dkt. Abel Nyamahanga katika sherehe za siku ya wanawake Duniani ambayo imeadhimishwa hapo jana katika uwanja wa Red Cross Muleba Mjini.

Dkt. Nyamahanga amesema watahakikisha wanafuatilia na kuzisimamia kaya zote za watoto wanaojilea wao wenyewe ili waweze kupatiwa msaada wa haraka ikiwemo wa malezi na mahitaji ya familia.
Afisa Maendeleo ya jamii Wilaya ya Muleba Bi. Edna Kabyazi amesema pia wameweza kutoa Misaada ya wa mahitaji katika Gereza la Muleba ambapo Misaada yote imegharimu zaidi ya shilingi milioni 8.6
