Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Rapa Wakazi Kumlipa Mbunge Wa Jimbo la Kigoma Mjini Revocatus Chipando @officialbabalevo , kufuatia kusambaza taarifa za uongo na za kashfa dhidi ya Mlalamikaji, ambazo zilidaiwa kuharibu heshima na sifa zake katika biashara na tasnia ya muziki ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na duniani kwa ujumla.
Katika hukumu iliyotolewa Machi 13, 2026, Mahakama imebaini kuwa taarifa zilizotolewa na Mshtakiwa dhidi ya Mlalamikaji zilikuwa za uongo, zenye madhara na za kashfa, na zimeathiri sifa na hadhi ya Mlalamikaji.
Kutokana na uamuzi huo, Mahakama imeamuru yafuatayo:Mshtakiwa atoe radhi hadharani kupitia vyombo vilevile vilivyotumika kusambaza taarifa hizo, Mshtakiwa amlipe Mlalamikaji fidia ya Shilingi milioni 100 za Kitanzania (TZS 100,000,000) kutokana na madhara yaliyosababishwa na taarifa hizo za uongo na za kashfa, Taarifa zote za uongo ziondolewe mara moja katika tovuti, mitandao ya kijamii, blogu, magazeti na chaneli za YouTube.
Pia, Mhtakiwa azuiwe kabisa (amri ya kudumu ya Mahakama) kusambaza tena taarifa za uongo au za kashfa dhidi ya Mlalamikaji , Kiasi cha fedha kilichoamriwa kulipwa kitatozwa riba ya asilimia 7 kwa mwaka kuanzia tarehe ya hukumu hadi malipo yatakapokamilik na gharama za kesi zitalipwa na Mshtakiwa.
Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Dar es Salaam na kuhitimisha rasmi shauri hilo kwa kumpa ushindi Mlalamikaji.
