Samwel Masunzu- Kibondo, KIGOMA
Baadhi ya wananchi mjini Kibondo wilayani Kibondo mkoani Kigoma wameomba kukamilishwa kwa barabara za lami zinazojengwa mjini Kibondo kutokana na kufungwa kwa kipindi kirefu kupisha matengenezo.
Baadhi ya waendesha pikipiki za kubeba abiria “Bodaboda” ambao wamesema barabara zinazojengwa zmefungwa kwa kipindi kirefu hivyo huathiri usafirishaji
Wamesema barabara hizo ni , moja ya kutoka shule ya sekondari Malagarasi kuelekea stendi ya mabasi na ya pili ni barabara ya Msasani kuelekea uwanja wa Taifa ambapo wamesema licha ya kulazimika kuzunguka lakini gharama ya nauli inabaki ile ile ambayo abiria wameizoea

Akijibu chagamoto hizo, Kaimu Meneja wa wakala ya Barabara za mjini na vijini TARURA wilaya ya Kibondo mhandisi Andrew Alfayo amesema zipo barabara tatu ambazo zinaendeleakujegwa.
Amezitaja barabara hizo kuwa ni ya halmashauri inayotambulika kama barabara ya Kibondo – Kumhama -Bunyambo ambayo sehemu ya barabara imeshakamilika na shughuli inayoendelea ni ujenzi wa mitaro ya maji, taa na alama za barabaani na kwa sasa wameruhusu wananchi kuitumia kwa mwendo wa wastani
Amesema pia barabara mbili za Malagarasi na Msasani au barabara ya Kumwai mkandarasi yupo eneo la kazi na ndani ya siku 10 hadi 14 wataruhusu zianze kutumika kwa mwendo mdogo wakati mitaro ya maji ikiendelea kujengwa.
