Nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, ameweka kadi zake zote mezani! Hatma yake ndani ya Old Trafford sasa inategemea jambo moja tu: Uwezo wa timu kushinda mataji.
Licha ya kuwa mhimili wa klabu tangu mwaka 2020, fundi huyu wa Kireno amefunguka kuwa anachotaka ni “ushindani.” Bruno amesisitiza kuwa bila ushindani wa kweli, hakuna nafasi ya kubeba ndoo, jambo ambalo ndilo kiu yake kuu.

Ofa ya Saudi Arabia: Bruno alikiri kukataa mshahara wa kufuru wa Pauni 700,000 kwa wiki (zaidi ya Shilingi Bilioni 2) kutoka Al Hilal msimu uliopita, lakini ofa hiyo bado ipo mezani!
Vigogo wa Ulaya: Kuna klabu kubwa zinanyatia saini yake na zinaweza kutumia kipengele cha kuvunja mkataba cha Pauni Milioni 57 (takriban Shilingi Bilioni 185).
Takwimu za Hatari: Msimu huu pekee, Bruno ameshaweka kambani mabao 8 na kutoa asisti 17 kwenye EPL.
Man United inapambana kumbakiza nahodha huyu, huku kukiwa na tetesi za kumuandalia mkataba mpya mnono zaidi. Lakini swali linabaki; je, pesa itatosha kumtuliza Bruno kama hakuna matumaini ya ubingwa?
