
Takriban watu 23 wameuwawa baada ya Ndege za kijeshi za Israeli kushambulia jengo la makaazi ya watu katika eneo la kaskazini mwa Gaza.
Vifo hivyo vimeripotiwa wakati mapigano yaliyoanza upya hivi karibuni katika ukanda huo yakionyesha dalili ya kutopungua.
Wizara ya afya inayosimamiwa na kundi la Hamas imethibitisha vifo hivyo na hospitali ya Al-Ahly imeeleza kuwa miongoni mwa watu hao waliouwawa kuna wanawake wanane na watoto wanane
Kwa mujibu wa huduma ya dharura ya wizara hiyo ya afya, shambulio la Israel limelenga jengo la ghorofa nne katika eneo la Shijaiyah, mjini Gaza huku vikosi vya uokoaji vikiripotiwa kuendelea kutafuta manusura chini ya kifusi.