Wakazi wa Halmashauri ya mji wa Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa Kuepuka kufanya shughuli za kilimo karibu na vyanzo vya maji ili kutunza mazingira.
Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira Kasulu Mjini (KUWASA) Mhandisi Goodluck Shefatia wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Nyansha.
Amesema tayari wamewasilisha ombi kwa wasimamizi wa maji Bonde la ziwa Tanganyika kufanya utafiti na kubaini visababishi vya uharibifu wa mazingira na namna ya kulinda mazingira karibu vyanzo vya maji.
Diwani wa kata ya Nyasha Bw. Lameck Anthony amesema shughuli za kilimo karibu na chanzo cha maji ya Mto Mgandazi, zimechafua maji na kuiomba Idara ya maji halmashauri ya mji Kasulu kujenga uzio wa chanzo hicho.
