
Baadhi ya wananchi katika Halmashauri ya Mji Tarime wilayani Tarime mkoani Mara wanadaiwa kuendelea kukaidi maagizo ya kutofanya shughuli mbalimbali karibu na vyanzo maji.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, ofisini kwake Afisa Mazingira wa halmashauri hiyo Patrice Boniphace, amesema kuwa pamoja na juhudi zilizofanyika, bado baadhi ya watu wanaosha magari, kulima, kuchimba mchanga, kuchenjua dhahabu na hata kujenga karibu na vyanzo vya maji.
Afisa huyo amefafanua kuwa shughuli mbalimbali karibu na vyanzo vya maji huruhusiwa kwa kuzingatia vipimo vya mto au kijito.
Ametolea mfano, kwa mto mkubwa kama Mori, shughuli zinatakiwa kufanyika umbali wa mita 60 kutoka mtoni, wakati kwa mito midogo na vijito ni umbali wa mita 30.