
Serikali imefanya ukarabati wa barabara na kujenga madaraja zaidi ya sita mkoani Mwanza yaliyokuwa yameathiriwa kutokana na mvua za El Ninno zilizonyesha mwaka jana hapa nchini.
Meneja wa wakala wa barabara nchini TANROADS mkoa wa Mwanza Bw. Ambrose Paschal ameambia Radio Kwizera kuwa kazi ya ukarabati na ujenzi wa madaraja hayo ilianza mwezi Novemba mwaka jana na inatarajiwa kukamilika Mwezi Novemba mwaka huu.
Awali wizara ya ujenzi ilieleza kuwa tathimini ya mwezi April mwaka jana ilionyesha kuwa mvua iliyonyesha ilisababisha uharibifu wa miundombinu ya madaraja na barabara na kuwa jumla ya bilioni 986 zilikuwa zikihitajika kurejesha miundombinu hiyo katika hali yake.