
Rais wa Kenya William Ruto amesema kuwa mageuzi makubwa ya kitaasisi yaliyofanywa na Umoja wa Afrika yanafungua fursa za biashara katika bara la Afrika, yakiashiria enzi mpya ya muunganiko wa kiuchumi.
Rais Ruto amesema hayo jana alipohutubia ufunguzi wa mkutano wa kilele wa Afrika wa Shirikisho la Wafanyabiashara Duniani uliofanyika jijini Nairobi.
Amesema kuunda upya mashirika mengi muhimu yakiwemo Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Uuzaji na Uagizaji Bidhaa ya Afrika, Taasisi ya Mendeleo ya Umoja wa Afrika pamoja na taasisi nyingi za kiuchumi za kikanda, kunaleta matumaini kwa Afrika, na kuweka msingi wa ustawi unaohimizwa na uwekezaji, ukuaji wa viwanda, utengenezaji bidhaa kwa ajili ya masoko ya kimataifa, na biashara.
Amesema matokeo ya mageuzi hayo ni kuwa kampuni za utengenezaji na kampuni changa za teknolojia za Kenya zinaenea barani kote, na kuonyesha imani kubwa kwamba mustakbali wa kiuchumi wa Afrika uko katika biashara na ushirikiano kati ya nchi za bara hilo.