Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, amesema serikali imeanza kuchukua hatua za kudhibiti vitendo vinavyotishia usalama na amani katika Mkoa wa Kigoma, baada ya kuibuka kwa taarifa za uasi na matukio ya uvunjifu wa amani katika maeneo kadhaa.
Amesisitiza kuwa usalama wa raia na mali zao ni kipaumbele, na kwamba vyombo husika vinaendelea kufanya kazi kwa karibu ili kubaini chanzo cha matatizo, kuwachukulia hatua wahusika na kurejesha utulivu.Mpina ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa za kiintelijensia na kuepuka kusambaza taarifa zisizothibitishwa, ili kuzuia hofu na taharuki isiyo na msingi katika jamii.
