Na Samwel Masunzu- Kibondo, KIGOMA
Halmashauri ya wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma kupitia wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA imesema kwa sasa barabara zote za mjini zinazojengwa kwa kiwango cha lami zitawekwa taa za barabarani ili kupendezesha mji huo hasa nyakati za usiku.

Meneja wa TARURA wilaya ya Kibondo Mhandisi Dickson Kanyankole amesema mkakati huo ni kuhakikisha mji wa Kibondo unakuwa na taa za kutosha zitakazoruhusu shughuli nyingine kufanyika hata majira ya usiku
Baadhi ya wakazi mjini Kibondo wamesema uwepo wa taa za barabani umesaidia pia kupunguza uhalifu kutokana na mwanga uliopo sambamba na kuwasaidia kufanya biashara ndogondogo kando ya barabara.
