Kuelekea kufanyika kwa msimu wa nne wa tamasha la Kijana Smart linaloandaliwa na Radio Kwizera, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi Bi. Kanyesha Faustine amezindua na kutangaza rasmi kaulimbiu itakayoongoza tamasha hilo mwaka huu.
Akizungumza katika kipindi cha Nje ya Dimba kinachorushwa na Radio Kwizera, Bi Kanyesha amesema kaulimbiu ya msimu wa nne ni “Daka Fursa”, huku akibainisha kuwa ujumbe huo unalenga kuwahamasisha vijana kutambua, kutumia na kuendeleza fursa mbalimbali zinazowazunguka ili kujijengea maisha bora na kuchangia maendeleo ya jamii.
Bi Kanyesha ameongeza kuwa maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri huku akiwakaribisha vijana na wadau mbalimbali kujitokeza kushiriki katika tukio hilo kubwa la vijana.
Tamasha la Kijana Smart linatarajiwa kufanyika Julai 25 mwaka 2026 katika wilaya ya Ngara huku likipambwa na michezo mbalimbali ikiwemo soka kwa wanaume na wanawake, Valiboli (Volleyball) na Michezo mingine.
