Msanii anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nyumbu Mjanja, ameendelea kuvutia mashabiki wengi kutokana na mtindo wake wa kipekee wa muziki pamoja na ujumbe wa kijamii anaoutoa kupitia kazi zake.
Nyumbu Mjanja ambaye pia ni Polisi Jamii, ameonyesha kuwa anaweza kuunganisha majukumu ya ulinzi wa jamii sambamba na kipaji chake cha muziki. Kupitia nyimbo zake, msanii huyo amekuwa akitoa burudani, elimu pamoja na kuhamasisha maadili mema kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Katika safari yake ya muziki, Nyumbu Mjanja amesema anatamani kufanya kazi kwenye moja ya lebo kubwa za muziki nchini Tanzania, ikiwemo Kings Music Records inayomilikiwa na Ali Kiba au WCB Wasafi chini ya Diamond Platnumz.
Kwa mujibu wa msanii huyo, ndoto yake ni kukua kimuziki na kufanya kazi na wasanii wakubwa ili kuifikisha sanaa yake katika viwango vya kimataifa huku akiendelea kuitumikia jamii kupitia nafasi yake kama Polisi Jamii.
Mashabiki wengi wameendelea kumpa moyo na kuamini kuwa juhudi, nidhamu na kipaji chake vinaweza kumfikisha mbali zaidi kwenye tasnia ya muziki wa Tanzania.
