Rais wa Albania Bajram Begaj amefanya ziara rasmi mjini Vatican City na kukutana na Baba Mtakatifu Papa Leo XIV kwa lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Albania na Vatican pamoja na kujadili masuala ya kimataifa.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Jumba la Kitume, viongozi hao walijadili hali ya kisiasa na usalama katika eneo la Magharibi mwa Balkani, pamoja na hatua za Albania za kujiunga na Umoja wa Ulaya.
Ziara hiyo pia imelenga kuonesha mshikamano na kuendelea kuimarisha ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pamoja kati ya pande hizo mbili.
Baada ya mkutano huo, Rais Begaj alikutana pia na Kardinali Pietro Parolin pamoja na Askofu Paul Richard Gallagher ambapo walifanya majadiliano zaidi kuhusu ushirikiano wa kidiplomasia na maendeleo ya eneo la Balkani.
