Na Samwel Masunzu- Kibondo, Kigoma
Kanisa la Tanzania Asseblies of God T.A.G Agape Kibondo Mjini wilayani Kibondo mkoani Kigoma limeahidi kulipa gharama kwa mtu yeyote aliye tayari kusoma masomo ya ualimu wa watoto kwa lengo la kuongeza nguvu katika kuwafundisha watoto maadili mema.
Mchungaji wa Kanisa hilo Robert Luhumbi amesema hayo akiwa mgeni rasmi katika sikukuu ya watoto T.A.G Taifa Juni 21, 2026 ambayo imefanyika kanisani hapo.
Mchungaji Luhumbi amesema kulingana na idadi ya watoto kuwa wengi, kuna haja ya kuongeza idadi ya walimu na kanisa lipo tayari kulipa gharama zote za masomo.

Sikukuu hiyo imetanguliwa na matukio mbalimbali ikiwemo bonanza la watoto, kuona wahitaji na kongamano la watoto huku mwalimu mkuu wa watoto hao Bi. Justina Anselum akiwataka wazazi kuwaunga mkono watoto katika kushiriki huduma mbalimbali za ndani na nje ya kanisa.

