Msanii na mtayarishaji wa maudhui, Eni Oluwa, ameripotiwa kuanguka usiku wakati wa kushoot video ya wimbo mpya “Nakwamini” aliofanya na Phina, tukio lililozua hofu miongoni mwa waliokuwepo eneo la tukio.
Kwa mujibu wa post iliyowekwa kwenye Instagram na akaunti ya@afriquechique, tukio hilo lilitokea majira ya saa 5 usiku wakati wa kushoot video hiyo.
Kwenye clip hiyo Eni anaonekana akiwa kwenye mafunzo ya jeshi na pamoja na wenzake wakifanya mazoezi magumu ya kupanda ngazi na kuruka upande wa pili.
Eni anayeonekana kuwa na uchovu mwingi anafanikiwa kupanda lakini anaporuka chini anatua vibaya na hivyo kuonekana amejeruhi mguu wake.
Watu walikuwepo eneo hilo wanamfuata na kuanza jitihada za kumsaidia.
Kwenye video hiyo, Afrique Chique ameandika: “Anaendelea vizuri na anaendelea na matibabu, bila shaka atakuwa sawa, lakini nikaona niliweke hili hapa. Mafanikio hayaji kwa bahati tu! Kabla ya kuwaonea wivu au kuwashambulia watu maarufu, jiulize kama unaweza kuweka juhudi na kujitoa kwa kiwango ambacho baadhi yao hukifanya.”
