SANTA CLARA, CALIFORNIA - FEBRUARY 08: Bad Bunny performs onstage during the Apple Music Super Bowl LX Halftime Show at Levi's Stadium on February 08, 2026 in Santa Clara, California. (Photo by Kevin C. Cox/Getty Images)
Msanii wa Puerto Rico Bad Bunny ameweka rekodi kwa kufanya show ya mapumziko (halftime show) kwenye Super Bowl iliyovutia watazamaji wengi zaidi.
Kwa mujibu wa Complex, Hot 97 na vyanzo vingine kupitia takwimu za Nielsen, show hiyo imetazamwa na watu miliomi 135.4, na kuipuki show ya Kendrick Lamar iliyotazamwa na watu milioni 133.5.
Takwimu sasa zinasomeka kama ifuatavyo:
1. Bad Bunny (Super Bowl LX, 2026) — 135.4m
2. Kendrick Lamar (Super Bowl LIX, 2025) — 133.5m
3. Michael Jackson (Super Bowl XXVII, 1993) — 133.4m
4. Usher (Super Bowl LVIII, 2024) —123.4m
5. Rihanna (Super Bowl LVII, 2023) —121m
Ikimbukwe kuwa show ya Bad Bunny iliibua hisia mchanganyiko hasa baada ya raisi wa Marekani Donald Trump kuiponda show hiyo na kusema kuwa haikuvutia na ilikuwa haina ubunifu wa aina yoyote.
