Na Davis Donatus
Manchester United imemweka kiungo wa Italia na Newcastle United Sandro Tonali kwenye orodha ya wachezaji inaowafuatilia, kuelekea mpango wa kuijenga upya safu ya kiungo katika dirisha la usajili wa majira ya joto huko Old Trafford.
Kwa mujibu wa taarifa, Tonali anahitaji uhakika wa kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) kabla ya kukubali kujiunga na klabu yoyote.
Aidha, Ada ya uhamisho wake inatarajiwa kufikia pauni milioni 100, jambo linaloonyesha thamani na ubora wake katika soka la Ulaya.
Iwapo Manchester United itafanikiwa kufuzu Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, basi safi yao ya kiungo itakuwa hatari sana kwa wapinzani wake ikijumuisha wachezaji hawa;
1. Sandro Tonali ambae ni kiungo wa kati.
2. Kobbie Mainoo ambae ni kiungo wabkati pia.
3. Bruno Fernandez ambae ni kiungo wa kati mshambuliaji.
