Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema mkoa huo umejipanga kikamilifu kuhakikisha washiriki wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Umoja wa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) wanapata huduma zote muhimu kwa kipindi chote cha mashindano hayo.

Akizungumza leo Juni 9, 2026 wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ya kitaifa, RC Kheri amesema wananchi wa Iringa wanatambua umuhimu wa tukio hilo na wamejiandaa kuwahudumia wageni kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Amesema huduma muhimu pamoja na mazingira salama vinapatikana muda wote, huku akiwataka washiriki kuendelea kufurahia michezo na shughuli mbalimbali zinazoendelea katika viwanja vilivyotengwa kwa mashindano hayo.
