Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania inaendelea kushirikiana na nchi rafiki kuimarisha uzalishaji na usalama wa chakula kwa kuwa bado inategemea kilimo kwa kiasi kikubwa.
Rais Samia ameeleza hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumpokea na kuzungumza na Rais wa Singapore, Tarman Shan-mugarat-nam, aliyewasili nchini kwa ziara ya kikazi.
Pia Rais Samia amesema amezungumza na Rais wa Singapore, Tarman, kuhusu ushirikiano katika kuimarisha mifumo ya uhifadhi na usambazaji wa chakula pamoja na kuongeza uwekezaji katika sekta ya kilimo.
Aidha, Rais Samia amesema Tanzania imejipanga kuimarisha mageuzi ya kidijitali pamoja na matumizi ya majukwaa ya kidijitali kwa lengo la kukuza uchumi wa kisasa katika kipindi cha miaka 25 ijayo
