Na Davis Donatus
Rais wa FIFA, Gianni Infantino anatatarajiwa kukabiliwa na ukosoaji mkubwa wakati atakapohutubia kongamano la mwaka la Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA huko Brussels, Ubelgiji kesho Feb 12 Alhamisi.
Hii inajumuisha msimamo wake kuhusu marufuku ya Urusi , Uhusiano wake na Donald Trump na masuala mengine ya kisiasa.
Infantino amekosolewa kuitisha mabadiliko ga marufuku ya Urusi, huku wengine wakidai kuwa hatua hiyo ni ya kuwatendea vibaya wananchi wa Ukraine.
Urusi ilipigwa marufuku michezoni tangu ilipoivamia Ukraine mwaka 2022, lakini Rais huyo hivi karibuni aliomba marufuku hiyo iondolewe .
Pia amekosolewa kwa uhusiano wake na Trump, ambapo baadhi ya wanachama wa UEFA wakidai kuwa uhusiano huo unaathiri uamuzi wake.
Kongamano la UEFA ni tukio muhimu kwa soka la Ulaya, na hotuba ya Infantino itakuwa ikifuatiliwa kwa karibu na wajumbe na anatarajiwa kujadili masuala mengine kama Kombe la Dunia 2026 na nafasi ya UEFA katika soka la dunia.
Je, unadhani hotuba ya Infantino italeta suluhisho la kisiasa na kimichezo katika mataifa haya mawili Urusi na Ukraine?
