Takribani watu 20 wamefariki dunia huko Madagascar kufuatia kimbunga kilichosababisha upepo mkali ulioharibu mapaa ya nyumba na kusababisha mafuriko.
Mamlaka ya kusimamia majanga imesema watu 15 hawajulikani walipo na angalau wengine 33 wamejeruhiwa. Kimbunga Gezani kilitua Madagascar jana Jumanne katika mji wa pili mkubwa Toamasina, huku upepo ukipiga kwa kasi ya kilomita 250 kwa saa.
Wakaazi wa mji huo wameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa, upepo huo mkali umesababisha kuta za mawe kuanguka.
Kiongozi mpya wa nchi hiyo Kanali Michael Randrianirina aliyechukua mamlaka mwezi Oktoba, alikuwa mjini humo kutazama hali na uharibifu uliofanyika.
