Na William Mpanju- Biharamulo, Kagera
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo SACP Advera Bulimba amewataka madiwani wa halmashauri ya Wilaya Biharamulo kusimamia miradi ya maendeleo ya wananchi.
SACP Bulimba ameeleza hayo baada ya serikali kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya sekta ya elimu, afya, maji na barabara ambayo madiwani wana dhamana ya kuisimamia ili iwanufaishe wananchi.

Aidha amewataka madiwani kuhakikisha wanahimiza wazazi na walezi kuwapeleka shuleni wanafunzi ambao hawajaripoti tangu shule zifunguliwe ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya Biharamulo Bw Aprinary Mugarula amesema maelekezo ya Mkuu wa Wilaya madiwani watayasimamia ipasavyo ikiwemo na ukusanyaji wa mapato ya halmashauri na kubuni vyanzo vipya vya mapato.

