Msanii Mac Voice amesema kuwa makazi yake yalikuwa studio na hivyo alitakiwa kumvizia S2kizzy amalize kurekodi ndipo alale chini studio.
Ameyasema hayo wakati wa mahojiano, na Kamba hali hiyo ilimfanya atake kujua yeye kama msanii anaishije hivyo na wakati muziki wake unaingiza pesa na ndipo Rayvanny akampa majibu kwamba haingizi chochote anaitia Kampuni hasara.
Ameongeza kuwaaliingia kwenye show za Chaka to Chaka baada ya kukosa pesa ya matibabu ya mama yake, jambo lililomletea shida na label yake.
Amesema Rayvanny alimtumia Voice notes akimwambia “sitaki kukuona hapa studio,unajiona mjanja hii simu utaipiga sana” hali iliyomuogopesa msanii huyo na kuendelea kufanya show za Chaka to Chaka.
