Mamlaka ya Nigeria imesitisha safari zote za hija kwenda Israel mara moja, ikitaja wasiwasi wa kiusalama unaohusishwa na mzozo unaoongezeka Mashariki ya Kati.
Uamuzi huo ulitangazwa na Tume ya Kikristo ya Wahujaji wa Nigeria, chombo cha shirikisho kinachohusika na kuratibu mahujaji wa Kikristo.
Katika taarifa, tume hiyo ilisema hatua hiyo ni muhimu ili kuweka kipaumbele katika “usalama” wa mahujaji wa Nigeria.
Kusitishwa huko kunahusisha mipango yote ambayo tayari ilikuwa imeandaliwa kwa ajili ya safari za kiserikali na kibinafsi.
Safari hizo, ambazo mara nyingi hufadhiliwa au kuratibiwa na serikali za majimbo, ni sehemu muhimu ya kalenda ya kidini ya Nigeria.
Nigeria, taifa lenye watu wengi zaidi barani Afrika, lina idadi kubwa ya Wakristo, hasa kusini mwa nchi. Hija nchini Israeli inachukuliwa kuwa muhimu sana kiroho, huku washiriki wengi wakiweka akiba kwa miaka mingi ili kwenda safari hiyo.
