China imetangaza rasmi utayari wake wa kuwa mpatanishi katika mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati kufuatia kuongezeka kwa mvutano kati ya Marekani, Israel na Iran.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa China, Wang Yi, Beijing imesema iko tayari kuchukua jukumu la upatanishi ili kupunguza makali ya vita vinavyoripotiwa kusambaa katika maeneo mbalimbali ya ukanda huo.
China imeeleza kuwa suluhisho la kidiplomasia ndilo njia pekee ya kudumu ya kumaliza mgogoro huo na kuzuia athari zaidi kwa usalama wa kimataifa.
Hata hivyo, msimamo wa China umeibua mjadala wa kimataifa kutokana na uhusiano wake wa karibu na Tehran.
Hata hivyo Tangu kuanza kwa mvutano huo, Beijing imeonekana ikiunga mkono haki ya Tehran kulinda mamlaka na mipaka yake, huku ikizitaka Marekani na Israel kusitisha mashambulizi yao mara moja.

Kwenye picha ni Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi,
Kauli hiyo imeonekana kama ishara ya wazi ya kuunga mkono Iran, jambo linaloweza kuathiri taswira ya China kama mpatanishi huru katika mzozo huo tata.
Wakati mapigano yakiendelea na hofu ya kusambaa kwa vita ikiongezeka, mataifa mbalimbali yanaendelea kutoa wito wa mazungumzo ya haraka ili kuepusha janga kubwa la kibinadamu na kiusalama katika ukanda huo
