Serikali Ya Tanzania imesema tayari imeanza kazi ya ukarabati wa reli ya TAZARA ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha miundombinu ya usafirishaji nchini na kuongeza ufanisi katika sekta ya uchukuzi na biashara.
Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge inayosimamia sekta ya miundombinu jana Waziri wa Uchukuzi Makame Mbarawa amesema ukarabati wa reli hiyo utasaidia kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na abiria, sambamba na kuimarisha shughuli za kiuchumi kati ya Tanzania na nchi jirani.
Ameeleza kuwa maboresho hayo yataisaidia pia Bandari ya Dar es Salaam kufanya kazi kwa ufanisi zaidi, kwani reli hiyo ni kiungo muhimu katika kusafirisha mizigo kutoka bandarini kwenda maeneo mbalimbali ya ndani ya nchi pamoja na nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.
Aidha, amesema kwa sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa meli nne kwa wakati mmoja, hatua inayolenga kuimarisha usafiri wa majini na kuongeza uwezo wa kusafirisha abiria na mizigo katika maziwa makuu ya nchi
