Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma imewataka wachimbaji wa madini kuzingatia sheria za utunzaji wa mazingira kwa kuepuka kukata miti hovyo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa amesema hayo baada ya kufika kitongoji cha Mowago ‘B’ kata ya Kasanda eneo ambalo linasadikiwa kuwa na madini ya dhahabu.
Kanali Mallasa amesema shughuli za uchimbaji wa madini hazipaswi kuwa sehemu ya kuhatarisha maisha hasa ya wale waliopo jirani na maeneo ya shughuli hizo
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Ndaki Stephano amesema wataendelea kusimamia sheria za utunzaji wa mazingira ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
.
