Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela yenye makao Makuu Tengeru, Arusha, imesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Indian Institute of Techology IIT Madras kampus ya Zanzibar kwa lengo la kuimarisha ubunifu, biashara ya matokeo ya tafiti na maendeleo ya kampuni changa za teknolojia.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Profesa Maulilio Kipanyula
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Profesa Maulilio Kipanyula amesema Makubaliano hayo, yanalenga kuanzisha, kuendeleza na kulinda bunifu mbalimbali pamoja na kuchochea ukuaji wa kampuni changa za teknolojia zitakazosaidia kutatua changamoto za kijamii na kuchangia maendeleo ya kiuchumi.
amesema kwa kushirikana na IIT Madras Zanzibar wamelenga kufanya utafiti kwa pamoja na kuendeleza matokea ya ubunifu katika teknolojia kwani taasisi hiyo ya India inauzoefu wa muda mrefu kwenye tafiti na ubunifu wa kiteknolojia.
BOFYA HAPA CHINI KUSIKILIZA SAUTI
