Wananchi wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera wametakiwa kujiepusha na tabia ya kuchoma moto kwenye mapori na mashamba kiholela ili kuzuia madhara yanayoweza kutokea yakiwemo ya kijamii na kiuchumi kwenye mazingira.
Mkuu wa Idara Maliasili na Mazingira wa wilaya hiyo Bw. Athanasi Andrew ametoa rai hiyo wakati akiongea na Redio Kwizera, na kubainisha kuwa wananchi wanatakiwa kuomba kibali cha kuwasha moto ili hata ikitokea umekuwa mkubwa waweze kusaidiwa bila kutozwa faini.
Aidha Bw. Andrew amesema kuwa wazazi na walezi wanaowajibu wa kuwafundisha watoto madhara yanayosababishwa na moto unaowashwa nje ya nje.
Sanjari na hayo amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika kuzima moto na kuripoti matukio ya uchomaji moto yanayotokea kwenye jamii.
